Home Entertainment PWANI GOSSIP: SHIRKO ARUSHA JIWE GIZANI !!!

PWANI GOSSIP: SHIRKO ARUSHA JIWE GIZANI !!!

83
0

PWANI GOSSIP: SHIRKO ARUSHA JIWE GIZANI !!!

Producer mkongwe wa Bongo fleva Awadh Salim “Shirko” katika ukurasa wake wa facebook, ametumia fursa ya Kumtakia Msanii wa hip hop Kaa La Moto kheri njema ya kuzaliwa na kuambatanisha michano flani ikiwalenga baadhi ya wasanii wengine wa pwani.

Katika chapisho hilo lililosheheni sifa kwa Kaa La Moto, Shirko pia hakuwaacha salama wasanii wengine huku akitumia mfano wa Kaa La moto kama msanii mkongwe na mwenye bidii wa vitendo na kutupilia mbali madai ya baadhi ya wasanii wanaojiita wakongwe wa mziki wa pwani wanaojipiga kifua kwa kazi walizofanya zamani.

Kulingana na Shirko, anasema haina maana yoyote kujinadi kwa mafanikio ya mziki badala yake kuwaachia mashabiki kutoa sifa hizo, akitumia mfano wa Kaa La Moto ambae wiki za nyuma alitetemesha steji za hip hop kule Bongo na kupokea baraka za wasanii wengi akiwemo Mkongwe Profesa Jay.

Shirko amedai mafanikio ya Kaa La Moto yanajiongelea , tofauti na wasanii wanaojipiga kifua kua washafanya na kutimiza kila kitu katika sanaa ya pwani. Shirko alifuta madai hayo kwenye nukuu

 

….”..ili uwe legend, hupaswi kuwaambia watu umefanya nini na nini, ni sisi [mashabiki] tunaopaswa kukupongeza umefanya nini na nini…”

 

Kauli hii inajiri baada ya msanii Susumila wiki za nyuma kuandika kua yeye tayari ashafanya makubwa katika tasnia ya mziki tangu zamani hadi sasa na kufanikisha kila kitu alichokua anakimezea mate katika maisha yake.

Vilevile kwenye chapisho hilo, Mkongwe wa miaka 24 kwenye burudani hili, Susumila aliwapa tahadhari ya kiafya wale wote wanaomfatilia ndani nje , kua wataumwa na vichwa bure endapo watalazimisha vichwa vyao kuelewa hatua zake.

 

..”..ukisema unanifwatilia utaumia kichwa bure… i have achieved everything..” Susumila katika ukurasa wake wa facebook. Kauli ambayo ilionekena kuwachokonoa wapinzani wake.

Previous articleDele Alli Checks Himself in A Rehab Center
Next articleDIAMOND PLATNUMZ AND JOSE CHAMELEONE IN ONE SONG?

Leave a Reply