Home Entertainment Nikivaa Chupi watu wanapenda, Mbosso apigia mstari Mavazi yake!

Nikivaa Chupi watu wanapenda, Mbosso apigia mstari Mavazi yake!

102
0

Kama wewe ni mpenzi wa Bongo fleva, lazima itakua umekutana na ‘vituko’ jukwaani vya Wasanii hususan wanaofanya kazi chini ya nembo kubwa Afrika, WCB Wasafi.

 

Lakini tukiachana na vitimbi vya wasanii hawa vikiwemo balaa la kupanda stejini na majeneza, mashabiki wengi wamekua wakitamaushwa na mavazi ya Mbosso ‘Selemani’ Khan ambaye kwa mara kadha ameonekana stejini akiwa amevalia gauni, dera, na mavazi mengine yanayoegemea jinsia ya kike.

 

 

Lakini Mbosso mwenyewe hajaonekana kushtushwa na eti eti ya mashabiki lakini zaidi kuzidi kujisafisha kwamba hawezi ona aibu ya kuvaa mavazi yoyote ya kike kwa kile anachodai kua watu wanapenda sana avae hivyo wakati wowote.

 

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa, Mbosso ameweka wazi utofauti wake akiwa stejini na akiwa mitaaani.

 

“..sioni aibu yoyote na ikitokea nivae chupi ya kike nitavaa sana…watu wanapenda nikivaa ivyo lakini huyo ni selemani jukwaani…. ukikutana na mimi njiani nabadilika kua Mbosso Khan, huyu mwenye anaongea sai ni Mbosso na yule wa madera ni Selemani lakini yote kwa yote siwezi wacha kuvaa hivyo…”

 

Tukiachana na Zuchu, Mbosso ni miongoni mwa wasanii wa Bongo fleva ndani ya WCB waliolelewa na misingi ya dini ya kiislamu.

Previous articleAzimio’s Cracks: A Blessing in Disguise for Ruto?
Next articleA battle looms between SRC and MPs over Allowance Determination 

Leave a Reply